SIMBA HAKUWEPO WALA TEMBO WALA TWIGA..YUPO HUYU
leo mdau ya SK NETWORK ilikuwa saba saba akifwatilia mambo ya fulani fulani katika banda moja wapo maeneo hayo..katika ripoti yake mdau wetu amekiri kuwa sabasaba ya sasa imekuwa na bidhaa nyingi sana za kutoka china .mpaka bidhaa zili ambazo tumezoea kuziona kwa wajasiliamali wa kawaida kabisa kutoka sido na wachina pia wanazo..ingawa si vibaya lakini kwa maono yake na wadau wachache waliohojiwa wamekiri kuwa china inanguvu kubwa ya matangazo na wanaummoja kutuzidi watanzania kiasi kwamba wanapata watazamaji wengi kuliko hata mabanda mengine ya bidhaa za aina kama yao...mabanda ya watanzania sasa wengi wao wamekutwa wakiwa wemenyongonyea na wengine hawakaribishi hata wateja..na pia mpangilio wa bidhaa zao hauvutie mteja kuangalia mara mbili... kama kweli tunahitaji kuwa kwenye ushindani wa biashara na mataifa mengine kama Kenya na China ...basi inabidi tubadilike tuache kuweka vinyago na makatuni mlangoni wakichekesha wateja,,,bali tujitahidi kuweka bidhaa ,mabango ya kuvutia na wahudumu wachangamfu.Benki fulani fulani zimechukua vijana na kuwaweka barabaran kuhamasisha wateja jambo hilo si baya bali vijana hao muda mwengine wanageuka usumbufu pale unapokubali kuzungumza nao....Tembeleeni saba saba ya mwaka huu na uje na maoni yako na sisi tutayaweka hewani...