Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa
ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye
aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa
wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la
mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza
alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia
ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti
bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka
makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina
mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais anamamlaka ya
kumuamrisha waziri wa fedha aiondowe bajeti……kwa hisani ya global publisher.