Kutokana na afya ya mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari
kuendelea kuwa mbaya Jumuiya ya madaktari iliamua kumpeleka daktari huyo nje ya nchi
ili aweze kupata matibabu zaidi kutokana na hospitali umma
hapa nchi kukosa vifaa muhimu
ambavyo lati kama vingekuwepo basi dokta
asingepelekwa nje ya nchi.katika hatua nyingine hali ya utolewaji wa huduma
imezidi kudhorota kupita kiasi kwenye hospitali za umma kutokana na mgomo wa
madaktari kushika kasi na baadhi ya madaktari kufukuzwa kazi katika mikoa
ya mbeya,Mwanza na Kilimanjaro.
Serekali
yatolewa nje
Katika hatua nyingine madaktari wamegoma kuchukua
msaada wa serekali walioonyesha nia ya kutaka kumsaidia dr ulimboka gharama za
matibabu nje ya nchi..wamesima wao kama madaktari na wadau wa afya pamoja na
jamii imeshajipanga kusimamia matibabu ya dokta hivyo hawahitaji msaada kutoka
serekalini.
Wananchi
wasikitishwa
Wananchi mmoja ameaamua kuacha kuendesha pikipiki
ambayo ndo iilikuwa biashara yake kwa kuhofia kuwa kama akipata ajali kipindi
hiki cha mgomo basi angeshindwa kupata matibabu na kama ni kidonda kingeoza
.wengine walisikika wakisema kuwa wanasiasa ndo wamewafikisha hapa kwa kuwa wanaleta
siasa kwenye roho zao .Wakazidi kulaumu kuwa wamejiongezea posho wabunge na
madiwani huku madaktari,wanafunzi,walimu na wananchi kwa ujumla wa kitaabika kwa matatizo mbali mbali
ambayo yanaweza kutatuliwa kama wangeweka kipaumbele mambo ya muhimu kwanza.